MBEGU, MBOLEA GHUSHI HATARI- WATAALAMU

Wataalamu wameonya kuwa kuingizwa kwa mbegu ghushi na mbolea ambayo haijakaguliwa kumechangia kuongezeka kwa magonjwa na wadudu wanaovamia mimea na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima nchini.
Kutokana na hilo, serikali imewaonya wafanyabishara dhidi ya kuingiza nchini mbegu hizo kupitia mipaka mbali mbali humu nchini na kuwauzia wakulima.
Wakizungumza baada ya kuzuru kituo cha Pamoja cha mpakani eneo la Namanga kaunti ya Kajiado, bodi ya shirika la kutathmini ubora wa mbegu KEPHIS imeonya kuwa wahusika watakabiliwa kisheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa