OLUOCH APONGEZA KIKOSI CHAKE
Kocha mkuu wa timu ya mpira wa vikapu ya Chuo Kikuu cha Africa Nazarene, Michael Oluoch, amepongeza timu zake licha ya kupoteza mechi zao za kwanza msimu huu katika Ligi ya kuu wikendi.
ANU Panthers walipoteza mechi yao ya kwanza 43-53 dhidi ya Safe Spaces waliopanda daraja katika ligi kuu ya wanawake huku timu yao ya wanaume ya ANU Wolfpacks wakiangushwa 51-65 na mabingwa wa zamani KPA kwenye mechi ya ligi kuu ya wanaume.
Oluoch alikiri kwamba timu ya wanawake kwa namna fulani ilijiamini kupita kiasi.
Kwa upande wa timu ya wanaume, Oluoch alilaumu wachezaji wake kwa kuipa KPA nafasi ya kufungua uongozi haswa katika robo ya tatu.
Hata hivyo, Oluoch anasisitiza yote hayajapotea kwani wana wachezaji wachanga na ni mchakato wa kujifunza kwao.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































