IPITISHWE AMA IANGUSHWE?

Wabunge wanatarajiwa kuanza tena kujadili Mswada wa Fedha wa 2024 ambao umeibua hisia tofauti miongoni mwa Wakenya kutokana na msukumo wake wa kutaka kutozwa ushuru zaidi.
Jana jumatano wabunge waliendeleza mjadala kuhusu ripoti iliyotolewa na kamati ya fedha ya bunge la kitaifa Pamoja na mswada wa fedha huku baadhi yao akiwemo mbunge maalum John Mbadi wakitilia shaka marekebisho hayo kwa madai kwamba huenda kuna njama fiche.
Imetayarishwa na Janice Marete