WETANG’ULA ATOA WITO KWA POLISI, DPP
Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, ameendelea kuitaka idara ya usalama kuendesha uchunguzi wa kina kwenye mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Kasipul Ong’ondo Were, akitaka waliohusika kuwajibishwa mara moja.
Akiwahutubia wanahabari katika hifadhi ya Lee alikoongoza tume ya huduma za bunge kuomboleza kifo hicho, Wetang’ula ameshutumu mauaji hayo na kushinikiza uchunguzi wa kina.
Aidha, amesisitiza haja ya mageuzi kufanywa katika kitengo cha usalama wa wabunge.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































