MAKALA YA CHEMUSUSU YAZINDULIWA RASMI

Makala ya tisa ya Chemususu Dam Half Marathon yamezinduliwa leo jijini Nairobi kabla ya mashindano hayo yanayopangwa kufanyika Novemba 16 huko Baringo, Elgeyo Marakwet.
Waziri wa Michezo Kipchumba Murkomen amesema mbio hizo za nusu marathoni za Chemususu Dam , zinaleta mabadiliko chanya zaidi kama uhifadhi wa mazingira, kujenga utangamano na umoja miongoni mwa jamii.
Lengo kuu la mbio hizo ni kuongeza uelewa wa changamoto za kimazingira huku kufadhili miradi yenye athari, ikiwa ni pamoja na kujenga njia ya kukimbia na madarasa mapya katika Shule ya Msingi Chemususu na kupanda miti 20,000 kila mwaka.
Pesa za zawadi kwa mshindi ni Kshs 250,000, Kshs 150,000 kwa mshindi wa kwanza na wa pili huku mshindi wa tatu akitia kibindoni Kshs 100,000.
Imetayarishwa na Nelson Andati