BUNGOMA YAONGOZA KWA AKAUNTI HARAMU- RIPOTI
Ripoti ya msimamizi wa bajeti ya serikali imefichua kwamba serikali za kaunti kutoka magharibi mwa nchi na ukanda wa pwani ziliongoza katika kuendesha akaunti haramu za benki kati ya Julai Moja na Disemba 31 mwaka jana.
Kwenye ripoti hiyo, kaunti ya Bungoma inaongoza ikiwa na akaunti haramu 321, Migori 321 nayo Nyandarua ya tatu na akaunti 88.
Msimamizi wa bajeti Margaret Nyakang’o amesema kwamba hatua hiyo imekuwa changamoto kwa afisi yake kufuatilia matumizi ya fedha za umma, akizitaka kaunti kuhakikisha zinafungua akaunti na benki kuu pekee kwa mujibu wa sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































