HUENDA MAPATO YA KENYA YAKAELEKEZWA KWA MIKOPO, RIPOTI

Kenya ni miongoni mwa nchi 23 zinazotarajiwa kutoa zaidi ya asilimia 20 ya mapato yao kwa malipo ya deni la nje huku suala hilo likiendelea kusumbua utawala wa Rais William Ruto.
Ripoti ya hivi punde ya Debt Justice, mshirika wa shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu nchini Uingereza, Christian Aid inaonyesha Kenya itatumia asilimia 26.1 ya mapato yake ya ndani kulipa mikopo ya nje, ya nane kwa juu zaidi barani mwaka huu.
Angola inaongoza bara la Afrika kwa kuweka wakfu mapato ya ndani kwa ulipaji wa mikopo ya nje kwa asilimia 59.8, ikifuatiwa na Zambia kwa asilimia 43.5, Misri 38.8, Djibouti 37.8, Tunisia 31.4, Gabon 29.1 na Benin asilimia 27.3 3.
Ripoti hiyo iliyopewa jina la ‘Kati ya Maisha na Deni’, inaonyesha malipo ya madeni ya nje ya Kenya yameongezeka kwa kasi kutoka wastani wa asilimia sita ya mapato ya serikali kati ya 2008 na 2016, hadi kufikia asilimia 24 mwaka 2019 na angalau asilimia 26 mwaka huu.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi