#Local News

HUKUMU YA JAJI YAMUACHA BILA WALINZI

Huenda mzozo ukashuhudiwa baina ya serikali tendaji na idara ya Mahakama baada ya jaji wa mahakama kuu Lawrence Mugambi kupokonywa walinzi wake, siku moja baada ya kumpa hukumu ya miezi 6 gerezani kaimu inspekta mkuu wa polisi Gilbert Masengeli.

Akiwahutubia wanahabari, jaji mkuu Martha Koome amesema walinzi hao waliopokonywa bunduki na kuondolewa wikendi iliyopita, na kukosoa hatua hiyo ya idara ya polisi ambayo inakiuka sheria.

Hata hivyo, Koome amewahakikishia wakenya kwamba idara ya mahakama itaendelea kulinda utawala wa sheria.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *