AFUENI KWA KYLIAN MBAPPE

Nyota wa Real Madrid, Kylian Mbappe amelazwa katika hospitali nchini Marekani baada ya kuugua mdudu wa tumbo, miamba hao wa Uhispania walisema Alhamisi.
Mshambulizi Mfaransa Mbappe alikosa mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia la Klabu ya Real Madrid dhidi ya Al-Hilal siku ya Jumatano, sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza wa Xabi Alonso akiwa usukani.
Mchezaji wa timu B ya Madrid Gonzalo Garcia, 21, alianza badala ya Mbappe na kufungua ukurasa wa mabao kwa Real Madrid dhidi ya wapinzani wao wa Saudi Arabia.
Mechi ya pili ya Madrid katika Kundi H ni Jumapili Juni 22 dhidi ya Pachuca ya Mexico huko Charlotte.
Mbappe alimaliza kama mshindi wa Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya katika msimu wake wa kwanza akiwa Real Madrid akiwa na mabao 31 kwenye La Liga, lakini Los Blancos walimaliza msimu bila taji lolote.
Imetayrishwa na Nelson Andati