MAANDAMANO YA KUCO YASITISHWA KWA MUDA

Chama cha maafisa wa klinik KUCO kimesitisha maandamano ya kila jumanne ili kupisha mazungumzo.
Katika taarifa kwa vyombo vya Habari katibu mkuu wa kuko George Gibore amesema maandamano hayo yaliyoratibiwa kufanyika kila jumanne yamesitishwa kwa muda katika juhudi za kuafikiana na serikali kuhusu malalamishi ya maafisa hao wa klinik.
Gibore aidha amedokeza kwamba viongozi wa KUCO wameratibiwa kufanya vikao na maaafisa wa wizara ya afya na vile vile baraza la magavana leo hii katika juhudi za kutafuta mwafaka kuhusu mgomo wao ambao umedumu kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































