MWANGAZA KUFIKA SENETI KESHO

Spika wa bunge la seneti Amason Kingi ameitisha kikao maalum hapo kesho kwa lengo la kusikiliza mswada wa kumbandua gavana wa Meru Kawira Mwangaza, baada ya wawakilishi wadi kwenye kaunti hiyo kumbandua gavana huyo kwa mara ya tatu wiki jana.
Mswada wa kumbandua Mwangaza uliwasilishwa na naibu kiongozi wa walio wengi bungeni humo Zipporah Kinya, anayemtuhumu Mwangaza kwa madai ya ukiukaji wa katiba, utovu wa nidhamu na utumizi mbaya ya afisi.
Kupitia taarifa, Kingi amesema kwamba kikao hicho kitaanza majira ya 2:30 unusu katika majengo ya seneti.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa