OMTATAH AWAKOSOA VIONGOZI WANAOFUFUA SIMULIZI ZA KIKABILA

Seneta wa Busia Okiya Omtatah ambaye pia ni mkwanaharakati wa kutetea haki za binadamu amekashifu baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao kulingana naye wanajaribu kufufua simulizi za kikabila za mfumo wa kisiasa wa zamani wenye sifa ya ukabila.
Katika taarifa kwenye mtandao wa X, seneta huyo amesema kuwa nchi haipaswi kamwe kurudi nyuma kwa siku ambazo makundi ya kisiasa yalikusanyika kwa misingi ya kikabila.
Omtatah ameongeza kuwa wakenya wote wanapaswa kulinda jamii mpya isiyo na kabila iliyoainishwa katika katiba ya 2010 kwa kuunda nchi ambayo ni ya kabila moja ambayo ni kenya.
Imetayarishwa na Janice Marete