KAZI YA POLISI SIO KUUA NI KULINDA;IPOA
Mamlaka ya kutathmini utendakazi wa maafisa wa polisi IPOA imeanzisha uchunguzi kufuatia kifo cha mmoja wa waandamanaji Rex Masai anayesemekana kuawa kwa kupigwa risasi na afisa wa polisi wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha.
Ann Makori mwenyekiti wa IPOA amewashtumu maafisa wa polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi kuwatawanya waqandamanaji.
Viongozi mbali mbali na wakenya kwa jumla wameibuia hisia tofauti kufuatia mauaji hayo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































