“WAANZILISHI’ WA UDA WATOA KAULI KUHUSU MALALA

Saa chache baada ya chama cha UDA kumtimua Cleophas Malala kutoka kwa wadhifa wa kaimu katibu mkuu, baadhi ya wanachama wametangaza kukubali uamuzi huo na kupongeza uteuzi wa Hassan Omar.
Kupitia taarifa, wanachama hao wakiongozwa na Joe Khalende wamesema zoezi hilo limefanywa bila miegemeo, wakitaka ukaguzi wa ununuzi wa vifaa vya chama wakati wa uongozi wa malala kufanywa.
Aidha, wanachama hao wametaka kurejelewa kwa zoezi la uchaguzi wa mashinani ikiwemo Nairobi uliokuwa umesitishwa kutokana na vurugu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa