WAKULIMA BUSIA WAPINGA ETIMS
Wakulima wa miwa katika kaunti ya Busia wamepinga vikali agizo la mamlaka ya ukusanyaji ushuru KRA kuwataka wajisajili na mfumo wa ETIMS kabla ya kuruhisiwa kuuza miwa yao, wakitishia kung’oa zao hilo na kujitosa katika kilimo mbadala kufuatia agizo hilo.
Wakizungumza katika eneo la Busibwabo kwenye hafla ya uhamasisho kuhusu mfumo huo wa ushuru, wakulima hao wamesema mfumo huo utawaletea hasara kutokana na gharama ya juu wanayotumia kuzalisha miwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































