RUTO ATETEA HATUA YA KUWATUMA MAAFISA 1000 WA POLISI HAITI

Rais William ruto ametetea uamuzi wake wa kuwapeleka maafisa 1000 wa polisi nchini Hait kuongoza oparisheni ya kureshesha amani nchini humo, licha ya kuwa kenya inakabiliwa na utovu wa usalama kufuatia wizi wa mifugo katika maeneo ya North Rift.
Akijibu maswali kwa wanahabari katika kikao cha pamoja na rais wa marekani Joe Biden katika ikulu ya white house, ruto amesisitiza kwamba ni jukumu la kenya kuyasaidia mataifa mengine yanayokumbwa na misukosuko ya kiusalama.
Kwa mujibu wa Ruto jukumu la Kenya nchini Haiti halitatatiza mpango wa serikali wa kuwakabili majangili huku akiweka wazi kwamba serikali yake imewatuma maafisa wa usalama zaidi ya 3000 eneo la North Rift kukabili wahalifu huku shule 15 zikiendelea kukarabatiwa na nyingine 20 zikiwa zimefunguliwa baada ya kufungwa kutokana na utovu wa usalama eneo hilo.
Ruto vile vile amepuuza madai kwamba Kenya imekuwa ikishurutishwa na marekani kuchukua jukumu la Haiti.
Akitolea mfano wanajeshi wa kenya KDF 1000 wanaoshirikiana na jumuia ya mataifa kusini mwa afrika kurejesha utulivu nchini drc, ruto amesema kenya ilichukua uamuzi huo wakati ambapo serikali yake ilikuwa imeanza kuwakabili majangili katika maeneo ya kaskazini mwa bonde la ufa
Ameongeza kusema kuwa sio mara ya kwanza vikosi vya maafisa wa polisi wa kenya kushiriki oparisheni za kurejesha amanai katika mataifa mengine wakati ambapo kenya inaendelea kukabiliana na changamoto za ndani.
Kwa upande wake rais wa marekani Joe Biden amesema kuwa marekani inalenga kutatua mzozo uliopo na kwamba serikali yake itatoa mchango wa kiinterlegicia akiongeza kuwa swala la Haiti limetokana na msukumo wa haki na kwamba haliwezi kulinganishwa na oparisheni za awali ambazo marekani imekuwa ikitekeleza katika mataifa mengine.
Imetayarishwa na Janice Marete