JOHO AWAHAKIKISHIA WAFUASI WA ODM USAWA NA HAKI

Naibu kiongozi wa chama cha ODM Hassan Ali Joho amewahakikishia wanaowania uongozi katika chama hicho kwamba mikakati imewekwa ili kuimarisha haki na usawa katika uchaguzi wa viongozi wa mashinani
Kwa mujibu wa Joho uongozi wa chama hicho umetambua baadhi ya mapengo na dosari ambazo utatiza uchaguzi na mchujo huku akiahidi kwamba mabadiliko yatafanya ili kudumisha usawa katika chama
Kwa upande wake gavana wa migori Ochilo Ayacko amewataka wafuasi kudumisha umoja na ushirikiano kama njia mojawapo ya kuimarisha chama
Imetayarishwa na Janice Marete