MUDAVADI APENDEKEZA NYONGEZA YA FEDHA KWA WIZARA YAKE
Msimamizi wa maswala ya kigeni ambaye pia ni Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi ameitaka serikali kuongeza mgao wa fedha katika wizara yake.
Kwa mujibu wa Mudavadi wizara yake inahitaji fedha Zaidi ili kufanikisha shughuli zake kikamilifu.
Ameongeza kuwa serikali imefanikiwa kutia Saini mikataba mbali mbali na serikali za mataifa menginee Pamoja na sekta binafsi kwa manufaa ya raia.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































