#Local News

MWEZI WA WATOTO: WATOTO NAROK WAPATA AFUENI

Ni afueni kwa familia zilizo na kesi mahakamani zinazohusu Watoto katika kaunti ya Narok baada ya mahakama ya Narok kuzindua rasmi mwezi wa huduma na haki kwa Watoto ili kushughulikia kesi zao kama suala la dharura.

Hakimu mkuu wa mahakama hiyo Hezron Nyamberi, amehakikishia umma kwamba wahudumu wote wa mahakama wako tayari kushughulikia kesi hizo na kuwataka wazazi kuwa macho na wanao.

Kwenye uzinduzi huo, wakazi wametahadharishwa dhidi ya kujihusisha na visa vya ukeketaji.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *