#Sports

NZOIA SUGAR INALENGA USHINDI

Huku msimu wa Ligi Kuu ya Kitaifa wa 2024/2025 ukielekea katika kipindi chake cha mwisho, Nzoia Sugar FC inalenga ushindi katika mechi zao zote zilizosalia.

Kocha mkuu wa muda Peter Ginn alisema kuwa Sugar Millers watakuwa wamejikusanyia pointi katika pambano lao lijalo dhidi ya Mombasa United wikendi hii katika Uwanja wa Sudi mjini Bungoma.

Huku zikiwa zimesalia mechi mbili pekee msimu kukamilika, Ginn alisisitiza umuhimu wa kupata pointi zote zinazopatikana ili kuepuka tishio la kushushwa daraja.Mkufunzi huyo pia amepania kulipiza kisasi kipigo chao cha mkondo wa kwanza dhidi ya Mombasa United, ambao waliwacharaza 1-0 mapema kwenye kampeni.

Pia aliwataka wafuasi wa Nzoia Sugar FC kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Sudi kuishangilia timu hiyo.

Timu hiyo yenye maskani yake Bungoma kwa sasa inashika nafasi ya 14 kwenye jedwali ikiwa na pointi 36, pointi tatu pekee juu ya msururu wa kushushwa daraja.

Imetayarishwa na Nelson Andati

NZOIA SUGAR INALENGA USHINDI

MUFUTU APONGEZA KIKOSI CHAKE KWA USHINDI WA

NZOIA SUGAR INALENGA USHINDI

VILABU VYA PREMIA VYAVUNA PAKUBWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *