KUCCPS YATOA MATOKEO YA KUJIUNGA NA VYUO

Huduma ya kuwapa wanafunzi nafasi katika vyuo vikuu na vyuo vya kadri (KUCCPS) imefungua rasmi tovuti yao na kuwapa fursa wanafunzi waliofanya mtihani wa kitaifa KCSE mwaka jana kufahamu hatma yao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Nairobi, Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesema kuwa asilimia 85 ya watahiniwa wa KCSE waliopata C+ na zaidi walituma maombi ya kujiunga na vyuo, asilimia 76.2 wakichagua kozi za digrii huku wengine 11,991 wakichagua Diploma.
Wanafunzi wengi walituma maombi kusomea digrii, huku wa kike wengi wakituma maombi ya kujiunga na taasisi za kifundi
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa