AZIMIO WAKOSOA MSWADA WA FEDHA

Mswada wa fedha wa 2024-2025 unaendelea kukosolewa kufuatia madai ya kutaka kuongezea wakenya mzigo wa kulipa kodi zzaidi wakati ambapo wakenya wanaendelea kukabiliwa na hali ngumu ya Maisha.
Viongozi wa upinzani wakiukashifu mswada huo kwa madai kwamba wakenya hasa walio na mapato ya chini ndio ambao watakaoendelea kukandamizika zaidi iwapo mswada huo utapitishwa.
Kiongozi wa chama cha wiper kalonzo Musyoka na mwenzake wa DAPK Eugene Wamalwa wanasema mapendekezo ya mswada huo yanaonekana wazi kuwalenga wenye mapato ya kadri ya kuwanyima fursa ya kujiimarisha kiuchumi.
Aidha katika hali ambayo imeonekana kuunga mkono mapendekezo ya baadhi ya viongozi wa eneo la mlima kenya wakiongozwa na naibu war ais Rigathi Gachagua katika mfumo wa one man one vote one shilingi katika ugavi wa raslimali , azimio inasema kuwa mfumo huo unalenga kuhakikisha usawa katika ugavi wa raslimali za kitaifa na wala sio ubaguziKwa upande wake kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa Opiyo Wandai ameitaja kodi mpya inayopendekezwa kwa wamiliki wa magari na bidhaa muhimu kama vile mkate kuwa inayolenga kupelekea kudorora kwa uchumi huku akilitaja bunge la kitaifa kusitisha mchakato wa ukusanyaji wa maoni na kuondoa kipengele hicho.
Imetayarishwa na Janice Marete.