MICHANGO YA PENSHENI YAPAA MARADUFU

Wakenya walio katika mipango ya pensheni wameongeza michango yao karibu mara mbili ndani ya miaka mitatu, kulingana na ripoti ya Mamlaka ya RBA.
Takwimu zinaonyesha ongezeko kutoka shilingi bilioni 62.73 kwa nusu mwaka ulioishia Juni 2022 hadi bilioni 118.80 kufikia Desemba 2024.
Mwaka 2024, iliongezeka zaidi hadi bilioni 116.10 nusu ya kwanza, na bilioni 118.80 nusu ya pili.
Wakati huohuo, michango kwa Hazina za Matibabu Baada ya Kustaafu (PRMFs) imeongezeka kwa kasi tangu Septemba 2024.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi