#Local News

PIGO ZAIDI KWA WASHUKIWA WA MAUAJI YA WERE

Washukiwa 2 katika kesi ya mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Kasipul Ong’ondo Were, akiwemo mkurugenzi wa mamlaka ya ustawi wa eneo la Ziwa Ebel Ochieng, wamepata pigo baada ya hakimu mkuu Irene Gichobi kukataa kujiondoa kwenye kusikiliza kesi hiyo.

Ombi hilo lililowasilishwa wiki jana wakimtuhumu hakimu huyo kwa upendeleo, ni pigo la pili kwao baada ya ombi lao la kutaka kesi hiyo ihamishiwe katika Mahakama ya Kibra au Milimani pia kutupiliwa mbali.

Upande wa mashtaka sasa una muda wa kuomba siku zaidi za kuwazuilia huku uchunguzi ukiendelea.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *