#Local News

SAKAJA AZINDUA UJENZI WA UWANJA WA KIHUMBUINI WA KSH.277 MILIONI

Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja amezindua ujenzi wa uwanja wa michezo wa Kihumbuini, mradi utakao gharimu shilingi milioni 277.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua mradi huo Gavana Sakaja amesisitiza kuwa uwanja huo utajengwa kwa viwango vya kimataifa, ikilenga kuimarisha soka jijini Nairobi.

Sakaja aidha ameangazia kuwa uwanja huo pindi tu utakapokamilika utachangia katika kuongeza mapato ya kaunti vile vile kuchochea biashara za mashinani karibu na uwanja huo.

Kuhusu athari za kifedha za miundombinu ya michezo, Sakaja amebainisha kuwa Kaunti ya Nairobi kwa sasa inapata zaidi ya shilingi milioni moja kila mwezi kutoka kwa Uwanja wa Dandora, ambao huandaa mechi za ligi ya soka ya Kenya.

Imetayarishwa na Janice Marete

SAKAJA AZINDUA UJENZI WA UWANJA WA KIHUMBUINI WA KSH.277 MILIONI

TUWATUNZE WANYAMA ;DKT ALFRED MUTUA

SAKAJA AZINDUA UJENZI WA UWANJA WA KIHUMBUINI WA KSH.277 MILIONI

SIMAMA NA FAMILIA YA REX MASAI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *