ATWOLI AMUONYA MBADI KUHUSU SERA ZA IMF

Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi COTU Francis Atwoli amemwonya Waziri wa fedha John Mbadi dhidi ya kutekeleza sera za shirika la kimataifa la fedha IMF bila kuzifanya tathmini ya kina, akisema sera hizo zinaweza kuwa na athari kubwa kwa uchumi wa nchi.
Katibu huyo amesisitiza kuwa kutekeleza sera za IMF zimewaathiri wananchi katika siku za hapo awali, na kuongeza kwamba ni vyema Mbadi aweke kipaumbele kwa mwananchi wa kawaida kabla ya kutekeleza sera zozote.
Kauli ya Atwoli imejiri siku moja baada ya Mbadi kufanya kikao na mwakilishi wa IMF hapa nchini Selim Cakir.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa