MAHAKAMA YAZIKA SHERIA YA SERIKALI

Mahakama ya rufaa imetia msumari wa mwisho kwenye jeneza la serikali, baada ya kudumisha uamuzi wa mahakama kuu kwamba sheria ya fedha ya mwaka 2023 ni kinyume na katiba, ikisema kwamba mchakato wa kuitengeneza sheria hiyo ulikuwa na dosari.
Kwenye uamuzi wake, majaji Kathurima M’inoti, Agnes Murgor na John Mativo wamesema mchakato huo ulikiuka vipengee vya 220 na 221 vya katiba na vipengee kadhaa vya sheria ya usimamizi wa fedha za umma na bajeti, na hivyo ni haramu.
Kwa mujibu wa majaji hao, katiba ilianza kukiukwa wakati ambapo sheria ya ugavi wa mapato iliidhinishwa kabla ya makadirio ya bajeti kuwasilishwa bungeni na Waziri wa fedha.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa