AZMA YA GOR MAHIA KUTWA TAJI YAPATA PIGO

Azma ya Gor Mahia kuhifadhi taji la Ligi Kuu ya FKF ilipata pigo kubwa baada ya sare ya 1-1 na wapinzani wao AFC Leopards katika mchezo mkali wa Mashemeji Derby Uwanja wa Raila Odinga mjini Homa Bay, Jumatatu.
Mabingwa hao wa rekodi ya ligi walikuwa wakitamani sana kupata pointi nyingi zaidi ili kusalia hai katika mbio za ubingwa.
Sare hiyo inawaacha Gor nafasi ya pili kwa alama 55, sita nyuma ya Police FC zikiwa zimesalia mechi mbili tu.
Polisi sasa wanahitaji pointi moja pekee kutoka kwa mechi zao zilizosalia dhidi ya Shabana na Gor ili kunyakua taji lao la kwanza kabisa la ligi.
Kocha Zico sasa ametupa taulo, akikiri taji hilo huenda likaelekea kwa Kenya Police FC.
Matumaini ya Gor ya ubingwa sasa yananing’inia, yakihitaji miujiza kutoka kwa Polisi wa Kenya na Tusker FC iliyo nafasi ya pili.
Imetayarishwa na Nelson Andati