HAZINA YA KITAIFA NJIA PANDA
Hazina ya kitaifa sasa inakabiliwa na hali ngumu ya kusawazisha matumizi ya nchi kwa mwaka ujao wa kifedha unaoanza wiki ijayo, kufuatia kuondolewa kwa Mswada wa Fedha wa 2024 wenye utata.
Uamuzi wa Rais William Ruto siku ya Jumatano kudinda kuidhinisha mswada huo kufuatia maandamano unaiacha Hazina ya kitaifa na pengo la shilingi bilioni 302 la mapato pale ambapo ilikua ifadhili bajeti ya shiligi trilioni 3.9 ya mwaka wa kifedha 2024/2025.
Mamlaka ya kukusanya Ushuru nchini (KRA) ilikuwa imepewa kiwango cha pesa cha kukusanya cha Shilingi trilioni 2.92 katika mwaka ujao wa kifedha, kutoka Shilingi trilioni 2.57 za mwaka unaokamilika ambazo huenda zikakosekana kwa angalau Shilingi bilioni 300.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































