POLISI FC YAPOTEZA FURSA YA KUIMARISHA UONGOZI KATIKA LIGI KUU YA KENYA

Polisi FC ilikosa fursa ya kuimarisha uongozi wake baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Nairobi City Stars jana Jumapili katika Uwanja wa Kenyatta – Machakos.
Matokeo hayo yaliacha Polisi kileleni na pointi 49, pointi moja mbele ya Tusker FC.
Mechi kati ya Gor Mahia na KCB iliahirishwa kutokana na mvua kubwa. Gor Mahia ina mechi mbili zaidi na pointi 43, pointi sita nyuma ya Polisi.
Shabana FC ilishinda Bandari FC 3-1 na kupanda hadi nafasi ya nne na pointi 40, huku Bandari ikishuka hadi ya tisa na pointi 36.
Imetayarishwa na Janice Marete