MWAMKO MPYA CHUONI MOI
Shughuli za masomo zinatarajiwa kuimarika katika chuo kikuu cha Moi na kutamatisha vuta nikuvute ambayo imekuwepo kwa miezi kadhaa, baada ya usimamizi mpya wa chuo hicho kuanza rasmi majukumu yake na kuahidi kuboresha huduma.
Baada ya mkutano na wafanyakazi wa chuo hicho, mwenyekiti Profesa Noah Midamba na naibu chansela Profesa Kiplagat Kotut wameahidi mageuzi ya kudumu chuoni humo.
Aidha, wameahidi kuwa wanafunzi watakuwa wakikamilisha masomo yao kwa wakati.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































