#Local News

WAITITU ASHITAKIWA KWA TUHUMA ZA KUTOA MANENO YA KUUTHI

Aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu ambaye ameshtakiwa kwa kutumia maneno ya kuudhi serikali amefunguliwa mashtaka.

Waititu alipinga kujibu mashtaka akisema mashtaka dhidi yake yalikuwa na dosari lakini Hakimu Mkuu Lucas Onyina amesema yalitolewa ipasavyo.

Kulingana na karatasi ya mashtaka, inadaiwa kuwa Waititu mnamo Septemba 29 katika uwanja wa Ruriru Kaunti ya Kiambu alitumia maneno ya matusi

Waititu anashutumiwa zaidi kwa kudai kuwa iwapo hoja ya kumtimua naibu wa rais itajadiliwa na kupitishwa Bungeni, nyingine inayotaka Rais aondolewe madarakani pia itawasilishwa na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka.

Hata hivyo, amekanusha mashtaka dhidi yake na kuachiliwa kwa dhamana ya Shilingi ksh50,000.

Kesi hiyo itatajwa tena Jumatano kwa ajili ya kesi ya awali.

Mahakama pia iliagiza afisa wa uchunguzi Andrew Ngowa aje na simu ya Waititu ambayo ilitwaliwa wakati alipokamatwa.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *