#Local News

MASAIBU YA GACHAGUA SI YA LEO, WAMUCHOMBA

Mbunge wa Githunguri Gathoni Wamuchomba ameibua madai mapya kuhusiana na masaibu ya kisiasa yanayomkumba naibu rais Rigathi Gachagua, akisema masaibu yake yalianza punde baada ya rais William Ruto kumteua Gachagua kuwa mgombea mwenza wake.

Akizungumza kwenye mahojiano na runinga moja nchini mapema leo, Wamuchomba amesema baadhi ya vigogo wa mlima Kenya walimpendelea Waziri wa usalama wa kitaifa Kithure Kindiki kuteueliwa kwenye wadhifa huo.

Kwa mujibu wa Wamuchomba, Rais William Ruto amekosa kutekeleza ahadi zake kwa eneo la Mlima Kenya, na kudai kwamba kuna njama ya kumbandua Gachagua.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MASAIBU YA GACHAGUA SI YA LEO, WAMUCHOMBA

KENYA YAAHIDI KUWATUMA POLISI ZAIDI HAITI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *