WAKO WAPI WANAHARAKATI MLIOWAKAMATA? OPIYO AULIZA POLISI

Kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa Opiyo wandayi amewalaumu maafisa wa polisi kwa kukamatwa kwa wanaharakati wanaodaiwa kuongoza maandamano ya kupinga mswada wa fedha.
Akizungumza katika bunge la kitaifa katika kikao kinachoendelea kwa sasa Opiyo ameilaumu serikali kwa kukamatwa kwa mwanabloger Gabriel Oguda kutokana na msimam o wake dhidi ya mswada wa fedha.
Opiyo vile vile ameibua madai kwamba kuna kikosi kimebuniwa cha kuwakamata na kuwahujumu wanahakakati wanaoongoza maandamano ya kupinga mswada.
Imetayarishwa na Janice Marete