MWANGA WA TUMAINI NGARA
Wakazi wa eneo la Ngara Railway Southern Zone wamepata afueni baada ya mahakama kuu kutoa agizo la kuzuia mpango wa kufurushwa kutoka makazi yao.
Kwenye kesi hiyo, wakazi hao, wengi wao wakiwa wafanyakazi wa zamani wa shirika la Reli na wakongwe, wanahoji kuwa wameishi katika eneo hilo kwa miongo ambako wamewalea Watoto na wajukuu.
Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 11 mwezi ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































