MGOMO WA UASU WANUKIA
Muungano wa kutetea maslahi ya wahadhiri UASU umetishia kwamba wanachama wake watagoma iwapo serikali haitatekeleza malalamishi yao kuhusiana na masuala mbali mbali ikiwemo kucheleweshwa kwa malipo yao.
Wakiongozwa na katibu wa muungano huo Maloba Wekesa, wahadhiri hao vile vile wameitaka serikali kutatua mgogoro wa uongozi katika chuo kikuu cha Nairobi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































