#Local News

WAUGUZI KISII KUSUSIA KAZI

Huenda wakazi wa kaunti ya Kisii wakakosa huduma za kimatibabu baada ya muungano wa wauguzi kwenye kaunti hiyo kutishia kugoma kutokana na madai ya serikali ya Kisii kukosa kutekeleza ahadi zake kwao.

Wakizungumza na wanahabari, viongozi wa muungano huo wamelalamikia hatua ya wenzao waliofuzu kukosa kupandishwa vyeo na kurejeshwa kazini kwa wenzao waliosimamishwa kazi miongoni mwa malalamishi mengine.

Hata hivyo, Waziri wa afya kaunti hiyo Ronald Nyakweba amewataka kuwa na Subira barua zinapoendelea kuandikiwa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAUGUZI KISII KUSUSIA KAZI

“SIWATAKI!”- GACHAGUA AWAAMBIA MAJAJI

WAUGUZI KISII KUSUSIA KAZI

MASOMO VYUO VIKUU KUSAMBARATIKA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *