NZIGE WANATISHIA MAZAO, LINURI ASEMA

Waziri wa kilimo Mithika Linturi amekiri kudorora kwa mazao ya kilimo kutokana na uwepo wa nzige zinazoathiri mimea, akitangaza juhudi za pamoja za serikali za kimaeneo kukabili changamoto hizo.
Kupitia ujumbe wake uliosomwa na katibu mkuu katika wizara hiyo Jonathan Mueke kwenye kongamano la mawaziri wa kilimo kutoka mataifa wanachama wa muungano wa kibiashara wa IGAD, Linturi ameelezea matumaini kwa suluhu kupatikana baada ya kukamilika kwa kongamano hilo.
Kwa upande wake, mkurugenzi wa shirika linalokabili nzige wa maeneo kame eneo la Afrika Mashirika Moses Mwesigwa, amerai kuimarisha mataifa wanachama katika vita hivyo, kauli iiliyokaririwa na Katibu mkuu wa IGAD Workneh Gebeyehu.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa