MBUNGE WA JUJA AKAMATWA NA DCI
Mbunge wa Juja kaunti ya Kiambu George Koimburi anaendelea kuhojiwa katika makao makuu ya idara ya upelelezi DCI baada ya kukamatwa ilia toe maelezo kuhusu matamshi yake kwamba serikali ilitumia shilingi bilioni 13 kwenye kampeni za aliyekuwa mwaniaji wa AUC Raila Odinga.
Kukamatwa kwake kumejiri muda mfupi baada yake kudai kuwa magari mawili aina ya Subaru yalikuwa yameegeshwa nje ya makazi yake katika eneo la Juja.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































