MAANDAMANO YA MATATU YAFUNGA NGONG ROAD
Shughuli za usafiri zimetatizika kwa mapema leo baada ya wahudumu wa matatu kufunga maeneo kadhaa ya barabara ya Ngong jijini Nairobi ikiwemo Dagoretti Kona na makutano ya Ring Road walipokuwa wakiandamana kulalamikia visa vya kuhangaishwa na maafisa wa polisi.
Kulingana na wahudumu hao, polisi wamekuwa wakiwaitisha hongo kabla ya kuwaruhusu kuendesha biashara zao, wakishinikiza hatua kuchukuliwa dhidi ya maafisa hao.
Imemlazimu kamanda wa polisi eneo la Kilimani Ben Kobia kuwashawishi kufungua barabara, na kuwataka kuwasilisha Ushahidi wa hongo dhidi ya afisa yeyote wa trafiki.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































