#Local News

RAILA AONDOKA NCHINI KUELEKEA UINGEREZA

Kinara wa azimio raila oodinga amefafanua ni kwa nini baadhi ya viongozi waliochaguliwa chini ya muungano huo wameandamana na rais William Ruto katika ziara yake ya marekani.


Katika taarifa Raila amesema viongozi hao walipata mwaliko kutoka kwa serikali ya marekani , miongoni mwa wanaazimio ambao waliandamana na rais Ruto ni gavana wa Homa bay Gladys Wanga , mwenzake wa Machakos Wavinya Ndeti na kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa Opiyo Wandanyi.


Taarifa ya raila inajiri wakati ambapo maswali yameibuliwa kuhusu ni kwa nini viongozi hao waliandamana na rais William Ruto , raila amewashauri viongozi hao kutumia fursa hiyo kuhakikisha kwamba wanaelewa maswala ya manufaa kwa wakenya.


Yakijiri hayo, Raila ambaye yuko nchini uigereza anatarajiwa kuhutubu katika chuo kikuu cha oxford , huku akitarajiwa kutumika fursa hiyo kuzungumzia nia yake ya kuwania wadhfa wa mwenyekiti wa tume ya umoja wa afrika.

Imetayarishwa na Janice Marete

RAILA AONDOKA NCHINI KUELEKEA UINGEREZA

NANI KAMUUA HASSAN?

RAILA AONDOKA NCHINI KUELEKEA UINGEREZA

RUTO KUKUTANA NA BARAK OBAMA LEO ALHAMISI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *