#Football #Sports

PATRICK KORIR ATEULIWA KAMA MSIMAMIZI WA MUDA WA FKF

Shirikisho la Soka la Kenya jana Jumanne lilitangaza kumwajiri msimamizi wa muda mrefu wa kandanda Parick Korir kama afisa mkuu mtendaji wake mpya.

Korir anachukua nafasi ya Barry Otieno, ambaye aliwasilisha kujiuzulu kwake jana jumanne, baada ya huduma ya miaka mitano.

kwenye taarifa shirikisho la FKF limesema “FKF imechukua hatua haraka kumteua Patrick Korir kama Mkurugenzi Mtendaji wa Muda mara moja. Patrick analeta tajiriba ya uzoefu katika soka ya Kenya, baada ya kuhudumu kama mwandishi wa habari, mratibu wa soka, na hivi majuzi, kama Mkurugenzi Mtendaji wa Nairobi City Stars.

Uelewa wake wa kina wa mchezo huo, pamoja na ustadi wake wa usimamizi, unahakikisha kwamba atajumuishwa haraka katika jukumu lake jipya, na hivyo kuruhusu usumbufu mdogo wa utendakazi wa FKF,”

Kabla ya kuteuliwa katika FKF, Korir alihudumu katika wadhifa sawa na Klabu ya Ligi Kuu ya Kenya, Nairobi City Stars.

Korir ni msimamizi mwenye uzoefu wa juu, na historia ya muda mrefu katika soka. Atashikilia jukumu hilo kwa muda huku shirikisho hilo likipitia njia yake kuelekea uchaguzi wa urais wa tarehe 7 Disemba.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *