KPA WAMETUA ZANZIBAR

Mabingwa watetezi timu ya KPA ya mpira wa vikapu kwa wanawake wametua visiwani Zanzibar kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu kwa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Wanawake Afrika Kanda ya Tano, zinazotarajiwa kuanza Jumapili hii.
Timu tisa zitachuana kuwania tiketi ya kwenda Dakar, Senegal mwezi disemba.
Kocha mkuu Anthony Ojukwu ana matumaini ya kutetea taji lao la Kanda ya Tano.
The Dockers iliweka historia mwaka jana kuwa timu ya kwanza ya Kenya kutinga fainali ya Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Wanawake Afrika mjini Alexandria, Misri.
Wawakilishi wengine wa Kenya ni Equity Hawks, na wote watakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Al Ahly ya Misri, APR ya Rwanda, na REG.
Michuano hiyo itatia komeo Jumamosi, Novemba 2.
Imetayarishwa na Nelson Andati