MUTURI HAKUFUTWA, OWINO ADAI

Hisia mbali mbali zimeendelea kutolewa kuhusiana na hatua ya rais William Ruto kumtimua waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi na kumteua mbunge wa Mbeere North Goerffrey Ruku Kujaza nafasi hiyo, mkuu wa kituo cha kitaifa cha mawasiliano, NCC Charles Owino akisema kuwa Muturi alijiuzulu wala hakufutwa ili kujinufaisha kisiasa.
Owino ameyasema haya kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, naye seneta wa Makueni Dan Maanzo akisema uteuzi wa Ruku kuwa waziri ni mwisho wa safari yake ya kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa