BINGWA WA MBIO ZA PARIS CHEBET ANASEMA YUKO IMARA
Bingwa wa Olimpiki ya Paris 2024 Beatrice Chebet anasema yuko imara kiakili na yuko tayari kwa mpambano wa mbio za mita 5000 za wanawake katika Ligi ya Diamond Golden Gala mjini Rome kesho.
Akizungumza huko Roma, Chebet amezizimisha gumzo kuhusu pambano lililotarajiwa na mshikilizi wa rekodi ya dunia Gudaf Tsegay.
Chebet alisisitiza kuwa anawaheshimu wapinzani wake wote.
Atakabiliana na safu ngumu inayojumuisha Freweyni Hailu wa Ethiopia na Nadia Battocletti wa Italia, mshindi wa medali ya fedha ya Olimpiki ya mbio za mita 10,000.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































