KENYA YAPOKEA MKOPO MPYA
Kenya imetia saini mkopo wa masharti nafuu wa $126.8 milioni kutoka hazina ya Kimataifa ya Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ili kufadhili mpango mpya unaolenga kuboresha maisha ya watu wa mashambani na kulinda maliasili.
Kulingana na waziri wa fedha John Mbadi, Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Maliasili (INReMP) unalenga kushughulikia uharibifu wa mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa, na kupungua kwa maisha katika maeneo ya mashambani mwa nchi.
Hazina ya Kitaifa imesema mpango huo utatekelezwa katika kaunti 10 ambazo ni Elgeyo Marakwet, Pokot Magharibi, Trans Nzoia, Uasin Gishu, Nandi, Kakamega, Kericho, Kisumu, Homa Bay, na Migori. Shirika la IFAD ni wakala wa umoja wa mataifa ambapo kazi yake kuu ni kukabiliana na umaskini na njaa katika maeneo ya mashambani ya nchi zinazoendelea.
Mkataba wa hivi karibuni unaongeza uzito katika taasisi ya kifedha nchini Kenya, ambalo linajumuisha miradi minne inayoendelea katika kilimo, ufugaji wa samaki, mifugo na ujumuishaji wa kifedha vijijini
Imetayrishwa na Maureen Amwai
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































