SERIKALI YA KILIFI YATOA AJIRA KWA VIJANA
Serikali ya kaunti ya Kilifi imetakiwa kuongeza nafasi za ajira kwa vijana wanaotaka kujisajili katika mpango wa kazi mashinani.
Mkurugenzi wa afisi ya mwakilishi wadi wa Sheila Mohamed Modein anasema kwamba vijana 58 pekee watanufaika na mpango wa kwanza katika awamu ya kwanza ya mpango huo katika eneo hilo.
Ameongeza kuwa mpango huo utapiga jeki juhudi za kukabili uhalifu miongoni mwa vijana.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































