MUSYOKA MAHAKAMANI KUPINGA MKATABA WA ADANI

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka hii leo anatarajiwa kuwasilisha kesi mahakamani kupinga mkataba baina ya serikali na kampuni ya Adani ya India unaolenga kuipa kampuni hiyo usimamizi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA kwa miaka 30.
Kwenye kesi hiyo, Kalonzo vile vile analenga kupinga mipango ya kuipa kampuni hiyo kandarasi ya kujenga mifumo ya kupitisha umeme, mradi ambao tayari dola bilioni 1.5 zimetolewa ili kuufadhili.
Kulingana na makamu huyo wa zamani wa rais, mpango huo umejaa siri na utaiweka Kenya hatarini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa