JOPOKAZI LA KUCHUNGUZA DHULUMA LAAPISHWA

Kitendawili cha mauaji yanayokisiwa kuwalenga wanawake kinatarajiwa kuteguliwa hivi karibuni baada ya jopokazi la kuchunguza visa hivyo chini ya uwenyekiti wa aliyekuwa naibu jaji mkuu Nancy Barasa kuapishwa. Mauaji hayo yameibua hofu nchini, takribani wanawake 170 wakiripotiwa kuuawa mwaka uliopita, katibu katika wizara ya usalama Raymond Omollo akilitaka jopokazi hilo kusaka suluhu mara moja. Kwa […]

UN MBIONI KUREJESHA UTULIVU DRC

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeandaa kikao cha pili kujadili hali tete iliyoko mashariki mwa taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Mkutano huo umeitishwa na viongozi wa DRC kutokana na mapigano ya kundi la waasi la M 23 ambalo limeuteka mji wa Goma na uwanja wa ndege. Waziri wa masuala ya […]

OGAMBA: SHULE ZIMEPOKEA BILIONI 19

Ni afueni kwa shule za msingi na upili za umma baada ya shilingi bilioni 19 kati ya bilioni 48 kutolewa ili kufanikisha shughuli za masomo shuleni humo, kufuatia lalama za walimu wakuu. Kwa mujibu wa waziri wa elimu Julius Ogamba, malimbikizi ya fedha hizo yatatolewa kufikia wiki ijayo. Ameyasema haya alipokuwa akikagua madarasa ya gredi […]

MANCHESTER UNITED YACHARAZA FULHAM 1-0

Ruben Amorim alikaribisha nadra ya kuweka lango safi wakati wa ushindi wa Manchester United wa 1-0 dhidi ya Fulham, lakini hakufumbia macho hitaji la timu yake kuboresha licha ya alama tatu muhimu. Goli la Lisandro Martinez lililopatikana baada ya mpira kugonga mchezaji mwingine lilimpa Amorim afueni kidogo, ambaye ameshinda mechi nne pekee kati ya 12 […]

KVF YATAFUTA KOCHA WA MALKIA STRIKERS

Shirikisho la Mpira wa Voliboli la Kenya (KVF) linatafuta kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya wanawake ya voliboli, Malkia Strikers, kuelekea Mashindano ya Dunia ya Wanawake ya FIVB 2025 yatakayofanyika kuanzia Agosti 22 hadi Septemba 7, mwaka huu nchini Thailand. KVF ilitangaza kuwa inakaribisha maombi kutoka kwa wale wanaopenda kushika nafasi ya kocha […]

KENYA POLICE YASHINDA MARA SUGAR NA KUREJEA KILELENI MWA LIGI KUU YA FKF

Kenya Police waliwalaza Mara Sugar bao moja pekee na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF) katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Awendo jana Jumapili. Clinton Kinanga, ambaye yuko kwenye fomu bora, alifunga bao muhimu katika dakika ya 56 na kuwafanya maafisa wa polisi kurejea kileleni mwa ligi wakiwa na pointi 36, […]

AFUENI: MATABIBU WASITISHA MGOMO

Ni afueni kwa wanaosaka huduma za kimatibabu katika hospitali za umma baada ya maafisa wakliniki kusitisha mgomo wao kwa siku 21 ili kupisha mazungumzo kuhusu malalamishi yao. Katika taarifa kwa wanahabari, katibu mkuu wa muungano wa maafisa hao George Gibore hata hivyo, amesema mgomo huo utaendelea katika kaunti za Kwale, Vihiga, Uasin Gishu na Lamu. […]

RUTO AWAKEMEA WANAOPINGA SHA

Rais William Ruto amewataka wakenya kupuzilia mbali wanaopinga mpango wa afya wa SHA na badala yake akawataka wajisajili kwa wingi ili kupokea ambacho serikali imetaja kuwa matibabu bora. Akizungumza kwenye kaunti ya Busia akiwa kwenye ziara, Rais amesisitiza kwamba chini ya mpango huo, wakenya watapata matibabu kwa gharama ya chini. Aidha, ametaja pingamizi dhidi ya […]

IKULU: HAKUTAKUWA NA KUPOTEZA AJIRA

Msemaji wa Ikulu, Hussein Mohamed, amesema hakuna mfanyakazi atakayepoteza kazi kufuatia uamuzi wa Baraza la Mawaziri wa kuunganisha mashirika 42 ya kiserikali yenye majukumu yanayofanana kuwa mashirika 20. Mageuzi hayo, yaliyotangazwa baada ya mkutano ulioongozwa na Rais William Ruto Kakamega, pia yanajumuisha kuvunjwa kwa mashirika tisa na marekebisho ya mengine ili kupunguza matumizi ya umma. […]

POLISI UINGEREZA WACHUNGUZA MAUAJI YA MWANAMKE MKENYA ALIYEPATIKANA AMEUAWA LONDON

Polisi nchini Uingereza wanachunguza tukio la mwanamke mwenye asili ya Kenya aliyepatikana amepigwa hadi kufa katika nyumba yake eneo la Woolwich, Kusini Mashariki mwa London. Taarifa ya Polisi wa Mijini imesema mwili wa Marianne Kilonzi, mwenye umri wa miaka 43, umepatikana katika nyumba yake baada ya wasiwasi kuhusu usalama wake kuripotiwa. Kulingana na wasifu wake […]