MBOLEA YA URUSI: SERIKALI YAVUNJA KIMYA

Serikali imepinga madai kwamba ilipokea mbolea ya bure kutoka kwa serikali ya Urusi na kisha kuipakia upya na kuwauzia wakulima nchini jinsi ilivyoibuliwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua.
Kulingana na katibu katika wizara ya kilimo Paul Rono, Urusi ilitoa tu malighafi magunia elfu 600 ya kutengeneza mbolea, nayo Kenya ikatoa kandarasi kwa kampuni moja ya humu nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa